Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka Machinga wote katika mkoa huo kuondoka katika maeneo ya barabara kutokana na usumbufu mkubwa unaojitokeza kwa kuwanyima haki watu wengine na kusababisha hali ya kiusalama kuwa mbaya.

Makonda amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake. Amesema kuwa kinacholiumiza jiji hilo ni wafanyabiashara kubwa kuwatumia machinga hao kukwepa kodi kwa kuwapa mizigo waliyohifadhi kwenye magodauni ili wawauzie kinyamela wakikwepa mkono wa Mamlaka ya Mapato Nchini.

Mkuu huyo wa mkoa amefafanua kuwa hali hiyo imepelekea kupungua kwa mapato kwa zaidi ya shilingi bilioni 800 katika mkoa huo. Hivyo, Makonda  ametoka siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kila Machinga anaenda sehemu stahiki na kuwapangia maeneo wale wote ambao hawana sehemu za kufanyia biashara.

Amesema kuwa lengo la Serikali kufikia mwaka 2017 kuwe na shemu ambazo wanachi wanapata bidhaa kwa uhakika na kwa utaratibu. Bofya hapa kuazama video

Shule ya Sekondari Almuntazir ya jijini Dar yapigwa faini mil. 25 kwa uchafuzi wa mazingira
Roberto Mancini Akunwa Na Kiwango Cha Balotelli