Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka maafisa elimu Jijini Dar es salaam kutoa taarifa nzuri ya maendeleo ya elimu ama kuandika barua ya kuacha kazi endapo watashindwa kuwasilisha taarifa hiyo.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa kikao chake na Maafisa elimu hao huku akiwataka kutoa ripoti ya maendeleo ya elimu katika Jiji la Dar es salaam.

“Nimesema kuwa mpaka kufikia jumatatu ni lazima kila mmoja alete ripoti ya maendeleo ya elimu katika sehemu yake, vinginevyo kwa atakaye shindwa kufanya hivyo aandike barua ya kuacha kazi,”amesema Makonda.

Majaliwa ashiriki mazishi ya mara ya pili ya baba mzazi wa Spika Ndugai
Watendaji Serikalini wapewa tahadhari kuhusu taarifa chafu