Makonda amepiga marufuku tabia iliyozuka katika baadhi ya maeneo jijini kwake ya kukamata na kuvizia bodaboda na kuwapiga bakora.

Amewataka wenye mamlaka ya kukamata bodaboda wenye makosa kutumia njia sahihi ya kukamata wahalifu hao kwani Dar es salaam sio mkoa ambao hauthamini utu.

Amesema kitendo hiko cha kuwapiga fimbo bodaboda ni kitendo ambacho kinahatarisha maisha yake na watu wanaoendesha katika eneo hilo.

”Mambo ya kuvizia bodaboda amekaa mahala anapita na pikipiki yake mnakamata mnapiga bakora marufuku, huu sio mkoa ambao hauthamini utu” amesema Makonda.

 

Kenyatta ashangazwa na kitendo cha mwanasheria mkuu kujiuzulu
Maamuzi kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi – Ligi daraja la pili

Comments

comments