Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuacha kupinga kila shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 19. 2 ambayo inatokea Kimara jijini Dar es salaam mpaka Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kuwa wapinzani hao wamekuwa wakipinga kila kitu bila kujali hata maendeleo ya sehemu husika yanayoletwa na rais John Pombe Magufuli.

”Niwatake hawa ndugu zetu waache kupinga kila kitu, kwa maana wao wamekuwa wakipinga shughuli zote za maendeleo, kwanza wao mpaka sasa wameshindwa kujenga hata makao makuu yao miaka nenda rudi, wamepanga mpaka leo, lakini wanapinga tu kila kitu,”amesema Makonda

Grace Mugabe aingia matatani, sasa atakiwa kukamatwa
Naibu waziri Mgumba asisitiza ushirikiano na Ueledi kazini

Comments

comments