Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewaonya wasichana wa mkoa wake wa Dar es salaam kutokubali kuolewa na wanaume ambao wanaishi katika maeneo ya bondeni ambayo ni hatarishi hasa katika kipindi cha mvua za masika.

Makonda amesema hayo alipofanya ziara katika eneo la Mbagala Kiburugwa na kuona baadhi ya nyumba za wananchi ambazo zimeathirka kutokana na kujengwa katika maeneo hatarishi na kuwataka wakazi hao kahama mara moja.

“Nitoe rai kwa wasichana ambao hawajaolewa, usikubali kuolewa na mwanaume ambaye atakuonesha ana kiwanja bondeni, kataa huyo sio wa kukuoa sasahivi angalieni akina mama mnavyotaabika na nyumba zimebomoka hujui watoto wako unawalaza wapi” amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa serikali haitaweza kutoa msaada wa chakula na malazi kila mara kwa wananchi ambao wanakumbwa na majanga yanayotokana na wao kuamua kukaa katika maeneo hatarishi kwa kujitakia.

Mkuu wa mkoa huyo amedai kuwa katika maeneo hayo ni ngumu kwa mwananchi kupata msaada wa dharura ikiwemo gari la wagonjwa au huduma ya zima moto.

Mama Kanumba ampa wakati mgumu Steve Nyerere
Dola 200 kulipwa kwa kina mama wanaonyonyesha