Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na wafanyabiashara kutoka China kujadilia namna ya uwekezaji.
 
Amesema kuwa kutokana na malengo yaliyo wekwa na Wizara ya TAMISEMI, kuwa kila mkoa uhakikishe unajenga viwanda 100, Wawekezaji hao watakwenda kuwekeza Tanga na kunduchi Jijini Dar es Salaam.
 
Aidha, ameongeza kuwa ujio wa wawekezaji hao ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wazawa kushirikiana nao ili kuweza kutanua wigo wa biashara.
 
“Sisi kazi yetu kama serikali ni kuweka mazingira ya uwekezaji, hawa ndugu zetu wametoka nchini China kuja kuwekeza nchini kwetu, kwa hiyo nawaomba wananchi watoe ushirikiano ili tuweze kuleta maendeleo,”amesema Makonda
 
 
 
 

 

Video: Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa yaiva
Video: Makamu wa Rais akagua mifereji Jijini Dar