Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametembelea kituo cha Jakaya Kikwete Moi katika hospitali ya Muhimbili akiwa na mwanamuziki maarufu wa bongo fleva Diamond Platnumz katika kampeni ya kuokoa maisha ya watoto 500 wanaosumbuliwa na magonjwa ya Moyo.

Katika ziara hiyo Makonda amewataka wasanii kuwa na moyo wa kutoa hasa kuwasaidia watoto wenye uhitaji kwani wao ndiyo viongozi wa kesho ambapo ametaja namba ya account itakayotumika kuhifadhi fedha zitakakazochangwa na watanzania ili kuokoa maisha ya watoto 500.

Katika hatua nyingine  Nasib Abdul ‘Diamond’ ameahidi kutibu watoto 10 ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa moyo huku akisisitiza wasanii kujitoa katika kusaidia jamii inayowazunguka,…Bofya hapa kutazama

LIVE BUNGENI: Tazama Maswali na Majibu, Bungeni Dodoma leo Novemba 6, 2019
Video: Kichere awatumia salamu 'mafisadi', Kilio upinzani

Comments

comments