Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka Waalimu Wakuu na Maafisa Elimu kutoa tathmini ya shule zote zilizochakaa jijini Dar es salaam ili aweze kuzikarabati.

Makonda amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waalimu Wakuu wa Shule pamoja na Maafisa Elimu. Amesema kuwa ni ajabu kwa shule za jiji la Dar es salaam kuonekana katika hali mbaya wakati wanauwezo wa kuzikarabati.

Pia, Makonda ametoa ahadi ya kugawa pikipiki kwa maafisa Elimu wa Kata ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Majaliwa atoa agizo TCU, NACTE
Spika Ndugai aridhia kuvuliwa uanachama Wabunge 8 CUF