Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutenga zaidi ya shilingi Bilioni 29 kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kila mwaka zitazopelekwa katika shule za msingi na sekondari kuratibisha shughuli za kielimu kuanzia ngazi ya mwalimu mkuu mpaka ngazi ya wanafunzi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ofisini kwake akidai kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa sera ya elimu bure.

“Pesa hiyo itatumika kulipia gharama ya elimu kuanzia posho ya walimu wakuu posho ya waratibu kata gharama za waendeshaji shule na kufanya kila mtoto wa kitanzania kwenda shule akiwa na unform na madaftari gharama zote zitatolewa na serikali” amesema Makonda.

Tazama video hapa chini.

HapoKale: 'Wenye kulamba' hadi kuwa Wanyiramba
Ajinyonga na kuacha ujumbe mzito