Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda anatarajia kugawa Kompyuta katika Halmashauri zote za Jiji la Dar es salaam ambazo zitatumika kuunda mfumo wa kuomba kutoa hati za ardhi pamoja na taarifa zote muhimu za wadau.

Ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi milioni 85 zilizotolewa na Kampuni binafsi ya Ulinzi ya Tamoba jijini Dar es salaaam, ambapo amesema Kampuni hiyo imetoa msaada huo wakati muafaka.

“Ninaishukuru Tamoba ambayo ni moja ya Kampuni za kizalendo zinazoguswa na maendeleo ya mkoa wa Dar es salaam, Kompyuta hizi sasa zinaenda lengo langu la kuhakikisha mkoa huu unakuwa na mfumo wa Kompyuta katika masuala yote,”amesema Makonda.

Aidha, amesema kuwa kupitia mfumo huo, mwananchi anayehitaji hati, atakuwa akiomba kwa kupitia mtandao na kupata majibu kupitia mtandao huo kabla ya kuandaliwa hati yake.

Hata hivyo, kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tamoba, Balozi Mstaafu Francis Mndolwa ametoa wito kwa wananchi wapenda maendeleo kujitokeza na kusaidia maendeleo ya mkoa wa Dar es salaam na kuachana na chuki binafsi.maendele ya mkoa wa Dar es salaam na kuachana na chuki binafsi.

Video: Uongozi NHC wamgusa Waziri Mkuu, atoa pongezi kwa utendaji wao
Chadema watinga Takukuru, wahoji madiwani wao saba kujivua uanachama