Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemteua, Hasheem Thabeet kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa viwanja 5 vipya vya mchezo wa Mpira wa kikapu maarufu kama Basketball.

Amesema viwanja hivyo vitakuwa ni vya wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ambapo kila wilaya kitajengwa kiwanja kimoja.

Ameongezea kuwa katika viwanja hivyo kutakuwa na fursa ya michezo  zaidi ya mitano ametaja michezo hiyo kuwa ni ngumi, mieleka, volleyball, Tennes na Basketball yenyewe vitakavyokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 3000.

Aidha tayari mchakato wa upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya ujenzi huo tayari umeshafanyika, ambapo wiki ijayo ramani ya viwanja hivyo itakuwa imekamilika tayari kwa kuanza ujenzi.

Habari kubwa zilizopewa uzito katika magazeti ya leo Juni 21, 2018
EXCLUSIVE: Tazama Kayumba akichambua wimbo wake wa 'mazoea'

Comments

comments