Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa kama itabainika kwamba msanii wa Bongo Fleva nchini, Harmonize anatumia kilevi aina ya bangi basi atamchukulia hatua kali za kisheria kwakuwa yeye ni mlezi wake.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wasanii mbalimbali ambapo alikutana na wasanii hao kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazo wakabili katika kazi yao ya usanii.

Amesema kuwa tayari amesha wasiliana na Gavana huko nchini Ghana, ili kuweza kumchunguza msanii huyo aliyepo nchini humo kubaini kama anatumia bangi ama sigara za kawaida.

”Ukiwa msanii ni lazima ujue kwamba wewe ni kioo cha jamii, na kwasasa tayari nimeshawasiliana na Gavana wa huko nchini Ghana ili kuweza kumchunguza Hamornise na ikibainika anatumia bangi, akitua tu hapa ni kumsweka ndani tu hakuna kingine,”amesema Makonda

Lissu auchokoza mkeka wa Ndugai, ‘sijawahi kulipwa senti’
Jeshi laapa kuilinda Serikali ya Bashir

Comments

comments