Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Samoe Abdallah kutoka mkoani Lindi anayedai kufika mbinguni, ameomba msaada wa kidunia ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

Ametoa ombi hilo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media mkoani Lindi, ambapo amesema kuwa baada ya kufika mbinguni alipelekwa katika tundu aliloingilia ili kuweza kuona maovu yanayotendeka duniani.

Amesema kuwa akiwa amelala nyumbani kwake, ghafla walitokea malaika wawili na kumbeba kumpeleka mbinguni ambapo alifikia kwenye nyumba nzuri na ya vioo ambayo hajawahi kuiona hapa duniani.

”Baada ya kufika kule mbinguni, nilikuta nyumba nzuri ambayo sijawahi kuiona hapa duniani, ilikuwa imejengwa kwa mawingu na sakafu ya mawingu, kwakweli naomba msaada wa kidunia kuhusu suala hili,”amesema  Samoe Abdallah

Basi la Frester lapata ajali Kagera
Wananchi wajichukulia Sheria mikononi Njombe

Comments

comments