Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa jana ambapo klabu ya Manchester City imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Feyenoord, Real Madrid imewachapa Apoel Nicocia kwa mabao 3-0 huku Liverpool wakibanwa mabavu na Sevila.

Manchester City walipata mabao kupitia kwa mlinzi wa kati John Stones aliyefunga mabao mawili dakika ya 2 na dakika ya 63 huku mabao mengine mawili yakifungwa na Sergio Aguero aliyefunga bao dakika ya 10 huku Gabriel Jesus akifunga dakika ya 25.

Kwa upande wa Real Madrid walipata mabao yao kupitia kwa Christiano Ronaldo aliyefunga bao la kwanza dakika 12 na bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 51 kabla ya Sergio Ramos kufunga bao la tatu dakika ya 61.

Sevilla waliibana mbavu Liverpool kwa kuwalazimisha sare ya mbili kwa mbili na wakati mabao ta Liverpool yakifungwa na Roberto Firminho na Mohamed Salah yale ya Sevilla yaliwekwa kimiani na Ben Redder na Joachim Corea.

Tazama mabao ya mchezo kati ya Liverpoo na Sevila hapa chini;

Dimitry Seluk kumtibua tena Guardiola?
Misa ya kumwombea Lissu yazuiliwa