Mwanamuziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) leo Januari 11, 2017 amekabidhiwa bendera ya Taifa, kwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano ya soka ya AFCON 2017, nchini Gabon.

Diamond ni miongoni mwa wasanii teule watakaotumbuiza katika hafla hiyo, ambapo Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa, Nape Nnauye wakati akimkabidhi bendera Diamond amesema kuwa, kuwepo kwa Diamond kwenye uzinduzi wa michuano hiyo ni kitendo cha kujivunia na kwamba Serikali ikishirikiana na DStv imefanya jitihada kubwa kufanikisha safari ya WCB kuelekea Gabon.

Diamond amempongeza kwa dhati Waziri huyo akieleza kuwa uwepo wake umechangia kwa kiasi kikubwa sanaa ya nchini kukuwa kwa kiasi kwa kasi huku akiwashukuru waandishi wa habari kutijitokeza kwa wingi katika tukio hilo

 

Watanzania kushuhudia michuano ya AFCON 2017 kupitia DSTV
Mbunge wa Chadema atupwa jela

Comments

comments