Wabunge wa upinzani wameamua kutoka nje ya bunge kwa style ya kuziba midomo. Hii ni kuonyesha mwendelezo wa kutokuwa na imani na naibu spika Dk. Tulia Ackson

Hii ikiwa ni mara ya tatu mfululizo mara baada ya kutangaza kuwa hawatahudhuria vikao vyote vinavyoongozwa na Dkt Tulia.

Wakiwa nje, Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia baada ya kutoka bungeni kwa staili ya aina yake akaongea haya

“Hii ni ishara ya kuonyesha hasira zetu, ni ishara yakuonyesha hatutokubali, ni ishara ya kuonyesha kwamba wakituzima midomo humu ndani nje kwa watanzania hawatatuzima midomo” – James Mbatia

Video: Maneno ya Mbunge Mbatia baada ya wabunge upinzani kutoka Bungeni
Ukawa watoka bungeni wakijifunga midomo, Mbatia afunguka