Serikali imetoa wito kwa wasanii nchini kurasimisha kazi zao ili kuweza kutambulika, kupata haki zao na kuongezea pato lao na la taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ubunifu wa vipaji na jinsi ya kuviendeleza.
“Sanaa inaongeza uelewa, sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana inayopelekea kukua kwa pato la taifa ingawa kuna changamoto kwa wasanii kutojitokeza au kujisajili ili kuweza kutambulika katika jamii”, amesema Wambura.
Ameongeza kuwa ili kutekeleza agizo la Rais wakati wa hotuba ya uzinduzi wa Bunge kuhusu haki za wasanii nchini,  Wambura amewataka wadau mbalimbali wa sanaa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha maslahi ya wasanii yanaboreshwa na kupinga uharamia wa kazi za wasanii                                                                

Aidha, Wambura amewataka wasanii kufuata Sheria, Kanuni na taratibu kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na masuala ya sanaa ikiwemo Tasuba, Basata, Cosota, Bodi ya Filamu ili kuwawezesha kufanya kazi kwa unafuu

Polisi wamtia mbaroni tapeli sugu Dar, aliwaliza viongozi wa dini, vigogo Serikalini
Video: Umasikini kwa wasanii Bhaasi..! Rais TCDB ataja mipango mikubwa