Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Majura Musiba amesema kuwa Mange Kimambi anatumiwa na FBI hivyo vyombo vya dola havitakiwi kumpuuzia bali vinatakiwa kumshughulikia kabla ya madhara hayajatoke kwa sababu amekuwa akiratibu shughuli mbalimbali za kutaka kuipindua serikali.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa amani ni kitu cha msingi katika taifa.

Amesema kuwa watu wenye nia mbaya ya kutaka kuharibu amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi na kwa kutumiwa na watu wa mataifa ya nje hawatakiwi kuvumiliwa hata kidogo kwani nchi ikipata machafuko, wao watakimbilia nje ya nchi na kuwaacha wananchi masikini wakitaabika.

“Mange Kimambi kwa taarifa zilizopo anatumiwa na shirika la Kijasusi la Marekani FBI, Mange Kimambi ni wa kushughulikiwa, nchi ikipata machafuko yeye anaendelea na shughuli zake za aibu anazozifanya huko, kwani nani hajui kwamba Mange anafanya shughuli hizo kwa Marekani na analipia kodi, kwa Marekani biashara hiyo inatambulika,”amesema Musiba

Video: Nchemba atakiwa kujitathmini utendaji kazi wake
Video: Hawa ni watu kumi hatari kwa usalama wa taifa letu- Musiba

Comments

comments