Muigizaji na mchekeshaji maarufu, Emmanuel ‘Masanja’ Mgaya amefikisha kilio chake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuomba awapatie wasanii wa mkoa huo fursa ya kupata viwanja.

Amesema kuwa idadi kubwa ya wasanii kwa sasa wanaishi katika nyumba za kupanga, kitu ambacho kinasababisha kushuka kwa thamani yao katika jamii.

Aidha, amesema kama utawekwa mpango wa kuwawezesha wasanii katika suala la makazi, wao wako tayari kujitengenezea mazingira mazuri yatakayowafanya waweze kulinda thamani yao katika jamii.

”Mkuu wa mkoa suala hili wala sio la kuongelea nyuma ya kamera kwasababu linamgusa kila mtu,” alisema Masanja.

“Wasanii wengi wanatamani kumiliki nyumba zao ili waondoke katika nyumba za kupanga, lakini tatizo letu wengi wetu hatuna viwanja vya kujenga nyumba, hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwetu, tunaomba utusaidie kwa hilo,”aliongeza.

Angalia video hii kupata undani wa ujumbe wa Masanja:

 

Kikosi Maalum cha Polisi chatua mkoani Njombe
Video: Diamond awashukia wasanii wanaopeleka hongo Wasafi TV

Comments

comments