Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amezitaka kamati zinazoshughulikia ucheleweshaji wa kesi kufika katika Magereza na kusikiliza baadhi ya kesi ambazo hazihitaji watuhumiwa wake kuwekwa magerezani.

Masauni ameyasema hayo alipotembelea Gereza la Butimba na kuzungumza na mahabusu ambao wana kesi zinazodhaminika huku wengine wakiunganishwa kwenye kesi za mauaji wakati hawajafanya mauaji hayo.

”Wakuu wa Magereza yote nchini wanatakiwa wawe wanafanya ziara kwenye Magereza ili kuweza kuzungumza na mahabusu, na wasipofanya hivyo, hatutaona umuhimu wao kubaki katika nafasi zao,”amesema Masauni

Video: Huyu mhandisi simtaki, hafai kabisa, kashatupiga pesa nyingi sana- Prof. Mbarawa
Waziri Mkuu ampatia shil. mil. 2.5 Mjasiriamali, 'Watanzania wanapaswa kujifunza kutoka kwako'