Mamia ya mashabiki wa rapa XXXTentacion wa Marekani aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumatatu wiki hii wamefunga barabara na mitaa ya Molrose Avenue na kufanya matukio yanayohatarisha maisha yao.

Mashabiki hao ambao wengi wao ni vijana walionekana walifurika taratibu mitaani na baadaye kuanza kupanda juu ya paa za nyumba kisha kujiachia hadi chini wakitua katikati ya umati uliokuwa umefurika jijini Los Angeles.

Kwa mujibu wa TMZ, vikosi vya jeshi la polisi vililazimika kutumia chopa (helicopter) kuzima vurugu zilizokuwa zinafanywa. Baadhi ya watu hao pia waliruka juu ya magari na kupiga kelele.

Rapa XXX aliuawa kwa kupigwa risasi Jumatatu kusini mwa Florida baada ya watu wawili wenye silaha kumfuata akiwa kwenye gari lake. Tukio hilo linadaiwa kuwa lilikuwa la ujambazi.

Kifo cha rapa huyo aliyekuwa ametengeneza rekodi nzito ndani ya muda mfupi kiliacha majonzi mazito kwenye kiwanda cha muziki wa rap.


XXX ambaye albam yake ya pili ya ‘?’ iliyotoka Machi mwaka huu ilishika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Top 200 aliwahi kusema kuwa endapo atakufa kabla hajatimiza ndoto zake, angependa kuona amesaidia mamilioni ya watoto wenye uhitaji wa elimu wasio na uwezo kutimiza ndoto zao.

Kocha wa Senegal: Timu ya Afrika itashinda Kombe la Dunia
Sugu: Mimi sio kama Roma, Nitaiburuza Basata mahakamani