Mashabiki wa Klabu ya Simba mkoani Kagera wameadhimisha siku ya ‘Simba Day’ kwa kuchangia Damu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Kagera ili kuwasaidia wagonjwa mbalimbali ambao watakuwa na uhitaji kuongezewa damu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa tawi la Kichwabuta lililopo Bukoba Mjini, Izidory Masawe amesema kuwa wameamua kuchangia damu kwa kuwa damu ni muhimu sana ukilinganisha na ajali zinazotokea na watu kupoteza damu nyingi.
 
Masawe amesema kuwa hilo ni zoezi endelevu ambapo mwaka jana pia walifanya hivyo ikiwa ni kujitoa kuhakikisha kwenye akaunti ya damu salama panakuwepo na damu ya kutosha.
 
Baadhi ya mashabiki wa Simba wa Tawi la Kichwabuta waliochangia damu wamesema kuwa damu waliyoitoa leo wanaimani itawasaidia wengi ambao watakuwa na uhitaji wa kuongezewa damu.

Wizara ya fedha kuiwezesha TRA kuongeza wataalam
Video: Ndege yaanguka, yateketea kwa moto Rufiji