Ugonjwa wa Saratani umekuwa ukiongezeka siku hadi siku duniani kote na ongezeko hilo ni kubwa zaidi katika  nchi zinazoendelea, takwimu zilizo tolewa na shirika la afya ulimwenguni zinaonyesha  kila mwaka  kuna ongezeko la wagonjwa  wapya milioni 14.1 wanaogunduliwa  na kati yao milioni 8.2 hufariki, vifo hivyo huwa ni asilimia 13 ya vifo vyote ulimwenguni kote.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisisi ya saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Oktoba 6, 2016 kuhusu matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi na kuchangia matibabu ya Saratani ya matiti siku ya tar 29 oktoba 2016.

Video: Waliovamia shule kuondolewa
Madudu uuzaji wa viwanja CDA, Waziri Mkuu atoa agizo