Polisi wanne wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya Wanaume Wamarekani weusi wawili ndani ya saa 48, Dallas, Marekani

Polisi wa Dallas Marekani wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo  pia wamesema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili kwa kulenga shabaha.

Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema Msako mkali unaendelea kuwasaka washambuliaji hao.

Polisi wengine saba wamejeruhiwa, wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo katika hali mahututi.

Risasi zilianza kufyatuliwa waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.

Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge jimbo la Louisiana. Hii hapa video inayoonyesha hali ilivyokuwa.

Jerry Muro: Nitakaa Kimya Kama Yanga Wataninyamazisha
DJ D Ommy, Millard Ayo, Harmonize watajwa kwa Mara ya Kwanza kuwania tuzo kubwa Marekani