Mshambuliaji Kylian Mbappe ameanza vizuri ligi ya Ufaransa ‘Ligue 1’ baada ya kufunga bao lake la kwanza katika mchezo ambao Paris Saint-Germain imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya klabu ya Metz.

Mbappe mwenye umri wa maiaka 18 atakayeigharimu PSG kiasi cha pauni milioni 166 msimu ujao ili kukamilisha uhamishi wa kudumu alipiga shuti kali na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wa kwanza akiwa na PSG.

PSG ambayo ina safu ya ushambuliaji ghali zaidi duniani inayoundwa na Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Mets ambao wanashika mkia katika ligi ya Ufaransa.

Tazama video ya goli la Mbappe hapa chini;

LIVE BREAKING: Serikali ikipokea taarifa madini yaliyozuiwa uwanja wa ndege DSM
Bashe aomba muongozo kuhusu uhakika wa maisha