Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, kupitia kwa Kamanda wake, Lazaro Mambosasa limesema kuwa linamsaka Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria mara baada kukaidi kusitisha maandamano yaliyopelekea kifo cha mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa, Mwenyekiti huyo alipanda jukwaani na kuwashawishi wafuasi wa chama hicho waandamane kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, kitu ambacho amesema ni kinyume cha sheria.

“Kuanzia sasa tunamsaka Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wa chama chake kuandamana na kupelekea kifo cha mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT,”amesema Kamanda Mambosasa

 

 

Serikali yajitosa kugharamia mazishi ya Akwilina
Polisi yatoboa siri ya mauaji kada wa Chadema

Comments

comments