Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid amepata nafasi ya kuuliza swali lake bungeni katika kipindi cha maswali na majibu leo Juni 15, Macho yake ameyaelekeza katika ugonjea wa Fistula ambayo ameutaja kuwa tatizo kubwa kwa wanawake kwani wanatumia gharama nyinyi kutibu ugonjwa huo , hivyo ameitaka Serikali kuona kuwatibia bure wale wote wenye tatizo hilo.

Serikali imetuletea majibu kuhusu kutibu bure ugonjwa wa Fistula

 fahamu kuhusu fistula

Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Inasababishwa na  kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na ana chanika  katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujivuia.
Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifunglia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni Sahihi mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ambapo unaweza kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati ni muhimu

Wapinzani Wa Young Africans Wafikiria Kujitoa Kombe La CAF
Video: 'Mbowe anawapigia simu Wabunge wakae kwenye chai badala ya kuingia Bungeni'-Mbunge Lusinde