Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutoa tamko juu ya viongozi ambao wamekuwa wakikiuka agizo lake la kutotoza ushuru wa mazao kwa wananchi wanaosafirisha chini ya Tani moja.

Ametoa ombi hilo alipopewa nafasi ya kutoa salamu mbele ya Rais kwenye mkutano wa hadhara kabla ya uzinduzi wa daraja la Magufuli katika Mto Kilombero, ambapo Lijualikali amesema kuwa wananchi wamekuwa wakikutana na kero hiyo licha ya Rais kupiga marufuku.

”Naomba Mh. Rais utoe tamko leo mbele ya wananchi wa Kilombero, ikiwa wewe umezuia kutoza ushuru wa mazao chini ya tani moja, Afisa Mtendaji ni nani mpaka akiuke, Mkurugenzi ni nani mpaka akiuke, basi leo toa tamko mbele ya wananchi,”amesema Lijualikali

Hata hivyo, baada ya kuanza kuhutubia wananchi wa Ifakara na Kilombero kwa ujumla Rais Dkt. Magufuli alipokea ombi hilo na kulifanyia kazi ambapo amesisitiza kuwa mtendaji yoyote atakayebainika kukiuka agizo hilo atawajibishwa mara moja.

 

 

Wataalamu wa afya waitaka serikali kuanzisha wiki ya chanjo ya mifugo
Video: Rayvany aiachia ngoma yake mpya 'Pochi nene'