Jijini Dar es Salaam, Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Mgosi amefunguka namna ambavyo wachezaji wa timu za mpira wanatumia imani za kishirikina kuroga ili kupata matokeo mazuri ya ushindi.

Amehadithia jinsi alivyoisaidia timu yake ya mpira kupata ushindi katika kombe la mbuzi lililoanzishwa mwaka 2015 ambapo ushindi wao ulipatikana baada ya yeye na wenzake wawili ambao walijiita kamati ya ufundi kwenda kuroga kwa mganga wa kienyeji aliyewapa masharti magumu ya nini wanatakiwa kufanya ili waibuke na ushindi.

”Niliagizwa nitafute kaburi la mwaka 1995 ili mechi yetu iwe nzuri, na nilitakiwa nifanye kazi hiyo mchana kila mtu anaona, baada ya kufukia kile kitu kwenye kichwa cha marehemu nilitakiwa nifukie na makalio, watu wakaanza kutukimbiza na kutuzomea” amesema Mgosi wakati anahadithia Mbanga hiyo

Jamaa amehadithia mwanzo mwisho katika kipindi cha Mbanga kinachorushwa kila jumamosi dar 24 kinachuhusu stori mbalimbali zisizosahaulika ambazo watu katika harakati za maisha wamezipitia.

Angalia hapa stori kamili.

Tabora yazalisha tani 52 ya asali kwa mwaka
Jeshi la Magereza lakanusha kauli za viongozi wa CHADEMA

Comments

comments