Wabunge wapenzi wa  Simba na Yanga walionyeshana makali yao katika mchezo uliofanyika kwenye kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Mchezo huo wa Wabunge wapenzi wa Simba na Yanga pamoja na mchezo mwingine wa wasanii wa Bongo Movie dhidi ya wasanii wa BongoFleva ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Katika mchezo huo Wabunge wa Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Wabunge wa Simba huku pambano hilo likiingiza jumla ya silingi milioni 187 ambazo ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko Kagera.

Nyumba za starehe, nyumba za ibada na baa marufuku mikesha, mwisho saa tano
Chadema wazungumzia hofu ya Lipumba kuvunja Ukawa