Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amedhihishia ulimwengu kuwa yeye ni bora zaidi baada ya kutajwa kuwa mshindi wa tuzo kubwa ya Ballon d’Or kwa mwaka 2015, usiku huu.

Messi amewamwaga Cristiano Ronaldo na Neymar da Silva Santos waliokuwa wakiisogelea tuzo hiyo ambayo mwaka jana iliingia mikononi mwa Ronaldo.

Ushindi huo umemuwezesha Messi kuvunja rekodi kwa kuwa mchezaji pekee aliyeshinda tuzo hiyo mara tano ikiwa ni mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.

Cristiano Ronaldo ameshika nafasi ya tatu akimfuati Neymar kwa mujibu wa kura zilizopigwa.

Picha: Jay Z na Beyonce walivyosherehekea ‘Birthday’ ya Binti yao
'Maalim Seif Sio Chama Cha Wananchi CUF'