Lioneil Messi amefunga mabao matatu (Hat-trick) katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Argentina imeupata dhidi ya Ecuador na kuiwezesha timu hiyo kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Wenyeji Ecuador walitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Romario Ibarra sekunde ya 38 baada ya mchezo huo kuanza lakini Argentina wakiongozwa na Messi walifanikiwa kusawazisha na kushinda 3-1 kwa mabao ya Messi aliyedhihirisha ubora wake hapo jana kwa kupiga Hat-trick.

Mabao ya Lioneil Messi yamemuweka kwenye vitabu vya rekodi vya Conimobel ambapo anakuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 21 wakati wa michezo ya kufuzu kwenye ukanda wa Amerika ya Kusini.

Tazama mabao yaliofungwa katika mchezo hou hapa chini;

Walimu wafeli mtihani wa wanafunzi darasa la kwanza, watimuliwa
Waajiri watakiwa kupima akiri za waajiriwa

Comments

comments