Meya wa jiji la Dar es salaam , Isaya Mwita, amewataka wazazi  wote  wa jijini Dar es salaam kushirikiana na kamati za shule ili kutatua tatizo la kufeli kwa  wanafunzi katika shule za Serikali mkoani humo.
Mwita ameyasema hayo februari 5, 2016 wiki katika ibaada iliyofanyika katika Kanisa la Ufunuo linalo ongozwa na Nabii Bendera lililopo Kimara Bonyokwa jijini Dar es salaam.
Amesema  ili kuongeza ufaulu kwa shule hizo nilazima wazazi waunangane kwa pamoja  na kamati za shule ikiwa ni pamoja na wazazi mmoja mmoja  kufuatilia Maendeleo ya watoto wao mashuleni.

” Ndugu zangu tusipo shirikiana katika jambo hili tutakuwa wa mwisho kila siku Sasa tubadilike ili  kunusuru watoto wetu” amesema Mwita.

 
Aidha amewataka waumini hao na watanzania kuiombea nchi na viongozi wake  ili Tanzania iendelee kuwa na amani,na watu wake waendelee kuishi kama ndugu bila kujali tofauti zao za dini, kabila na kisiasa.

Bulaya: Siasa isiingizwe kwenye vita ya madawa ya kulevya
Video: Data Vision International kudhibiti wizi mtandaoni