Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kwasasa anaunda mikakati ya kufungua fursa za uwekezaji wa kitalii jijini humo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kuna vitu vingi ambavyo watu wa Dar es salaam hawavifahamu.

Amesema kuwa utalii kwa jiji la Dar es salaam haukwepeki kwani linafukwe za kutosha na ndefu kuliko sehemu zote za miji ya Afrika Mashariki.

“Dar es salaam ni jiji moja linavivutio vingi sana, ni lazima tulijenge katika hali ya kitalii na kufungua fursa za uwekezaji wa kitalii,” amesema Mwita

Video: Wananchi wafunguka kuhusu hali ya kisiasa nchini
Video: Dkt. Bingwa wa magonjwa ya Mgongo Wazi na Vichwa Vikubwa aeleza chanzo