Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, Abdallah Chaurembo kesho afuatane na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Nassib Mmbaga hadi kwenye kiwanja kilichopo eneo la Matumbi na kukagua kama kuna uwezekano wa kuliongeza kwa taasisi ya Al-Hikma

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Juni 11, 2017 katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30 yaliyofanjia jijini Dar es salaa ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

Amemtaka Meya huyo pamoja na Mkurugenzi wampe majibu Jumanne kuhusu eneo hilo kwani limekaa wazi kwa muda mrefu licha ya kuwa walishaliomba na hawakupata majibu.

“Mstahiki Meya wa Temeke na Mkurugenzi wako, kesho Jumatatu nendeni mkaangalie eneo husika kama linafaa kuongezwa na mfanye maamuzi. Eneo hilo limekaa wazi kwa muda mrefu, na hawa wanataka wanataka kujenga zahanati. Jumanne asubuhi nipate taarifa ya maamuzi yenu,” amesema Majaliwa

Magazeti ya Tanzania leo Juni 12, 2017
Video: Majambazi wavamia mgodi, wajeruhi, wapora dhahabu na fedha