Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta leo amezindua rasmi mradi wa utekelezaji uboreshaji wa jiji la Dar es salaam, uliodhaminiwa na fedha za mkopo wa Benki ya Dunia ujulikanao kama Dar es salaam Metropoltan Development Project (DMDP).

Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo Makumbusho kata ya Kijitonyama kwa kusaini Mkataba na Mkandarasi Estim Construction, atakayetekeleza mradi huo awamu ya kwanza wenye thamani ya shil. bilioni 22 ndani ya mwaka mmoja kwa ubora wa kiwango cha juu.

Amesema kuwa mpango huo umelenga maeneo manne ambayo ni pamoja na uboreshaji miundo mbinu, kuinua makazi ya watu wenye vipato vidogo, kujenga uwezo na kusaidia usimamizi katika utekelezaji na tathmini.

“Nachukua nafasi hii kuwaomba wakazi wote wa kinondoni kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huu na kwa nafasi yangu, kwa niaba ya manispaa  napenda kuwahakikishia wote pamoja na mmradi huu tutaendelea na utekelezaji wa miradi mingine.”amesema Sitta.

Aidha mradi huu utakapo kamilika utasaidia kuondoa msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na kuongeza thamani ya makazi ya watu.

Ewura wapandisha bei ya umeme
Bondia Francis Cheka afungiwa