Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema kuwa viongozi wengi wa serikali wanapendelea upande mmoja wa msiba wa Akwilina kwani hata wao chadema wamekuwa wakipata misiba lakini serikali haitoi pole wala kuwafariji wafiwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa kada wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Daniel John.

Amesema kuwa kitendo cha viongozi wa serikali kutoenda kutoa pole katika familia ya Daniel John na kuegemea upande mmoja wa msiba wa familia ya Akwilina ni fedhea kubwa.

“Kwakweli hii ni fedhea kubwa sana kwa viongozi wa serikali kuegemea upande mmoja kwenye msiba wa Akwilina, hii si haki kwani wangekuja hata huku kutoa angalau salamu za pole na kuwafariji wafiwa, kwani kifo cha Daniel kinasikitisha sana,”amesema Jacob

 

Video: Milioni 80 kumzika Akwilina, Makubwa yafichuka kwa Kakobe
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 21, 2018