Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema kuwa viongozi wengi wa kiserikali hawajatenda haki katika msiba wa kada wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Daniel John.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuaga mwili wa marehemu huyo, ambapo amesema kitendo cha viongozi wa serikali kutoenda kutoa pole katika familia hiyo na kuegemea upande mmoja wa msiba wa Akwilina ni fedhea kubwa.

“Kwakweli hii ni fedhea kubwa sana kwa viongozi wa serikali kuegemea upande mmoja kwenye msiba wa Akwilina, hii si haki kwani wangekuja hata huku kutoa angalau salamu za pole kwa wafiwa,”amesema Jacob

Okwi aivusha Simba kombe la shirikisho Afrika
Video: Naibu Spika adai ana haki ya kikatiba kugombea ubunge

Comments

comments