Serikali ya Tanzania na Morocco zimetiliana saini mikataba takribani 22 ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara. Zoezi hilo limefanyika leo Oktoba 24, 2016 Ikulu jijini Dar es salaam.

Mikataba hiyo ya ushirikiano katika sekta ya kilimo, gesi, mafuta, reli ya Liganga na Mchuchuma na Sekta ya utalii imetiwa sani na ujumbe wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco ambao amewasili nao jana Tanzania katika ziara ya kikazi ya siku tatu. Ziara ya mfalme huyo ni kuimarisha  uhusiano baina ya Morocco na Tanzania.

Kabla ya zoezi hilo la kitiliana saini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI.

Rais Magufuli amesema kuwa kati ya mambo mbali mbali waliyozungumza wamekubaliana na Mfalme Mohamed VI wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa kisasa mkoani Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.

“Mbali na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza mambo mbalimbali na Mfalme Mohamed VI wa Morocco na nimemuomba atujengee Uwanja mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na thamani kati ya dola milioni 80 hadi 100 na amesema ataujenga, kwa hiyo utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam” – Rais Magufuli

Video: Tanzania na Morocco zatiliana saini mikataba 22
Video: Watu 400 kufanyiwa upasuaji wa mabusha bila malipo, Ilala