Tanzania  inatarajia kupokea ugeni mkubwa wa Mfalme wa Morocco, Mohamed  VI akiongozana na wafanyabiashara 1000, ambapo anatarajia kuwasili nchini Oktoba 23, 2016 saa 10.00 jioni na ndege sita kubwa pamoja na ndege ndogo mbili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius kambarage Nyerere Terminal 1.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ujio huo utakuwa na fursa kubwa kwa watanzania hivyo amewataka wafanyabishara kutumia fursa hiyo vyema kwani Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wawekezaji wanakuja nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
Makonda amesema pamoja na mambo mengine Mfalme anatarajia kusaini mikataba 11 ya kiuchumi na utalii itakayosaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hapa nchini. Bofya hapa kutazama video

Video: Magufuli amulika sakata la mikopo ya wanafunzi Chuo Kikuu
Video: 'Mikutano ya Yanga ni yakihuni' - Mzee Akilimali