Katika muendelezo wa ubunifu wa matumizi ya teknolojia ambayo yanarahisisha upatikanaji wa huduma bora na urahisi katika kukimu maisha ya Watanzania, mfumo wa Ada Lipa umezidi kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo sasa unawezesha watanzania kuwalipia ada watoto wao kidogo kigodo kupitia teknolojia ya kisasa ya ‘Kibubu’.

Mfumo huo uliobuniwa na Kampuni ya Datavision International wenye lengo la kuhakikisha watanzania wote wanapata haki yao ya msingi ya kupata elimu, umelenga kuwafikia na kuwawezesha watanzania katika hali zote kuweza kumudu gharama za masomo kwa kulipa ada kidogo kidogo.

Akizungumza na Dar24 Media, Ibrahim Stephano ambaye ni Meneja wa mfumo wa Ada Lipa, amesema kuwa kwa kutumia mfumo mpya wa kibubu cha Ada unaopatikana ndani ya mfumo wa malipo wa Ada Lipa, mzazi anaweza kuweka na kutunza fedha kidogo kidogo zitakazo tumika kulipa ada ya mtoto muda unapofika na kuepuka usumbufu wa kukatisha masomo ya mtoto.

Meneja huyo ameongeza kuwa mfumo unafanya kazi saa 24 na mzazi anaweza kuwa na vibubu vya watoto wote wake, hivyo mfumo huo umeleta ukombozi kwa wazazi wanaopata shida kulipa ada kwa mkupuo.

IGP Sirro atoa onyo, 'Ni bora mtoe ushirikiano'
Majaliwa akabidhi Jenereta kituo cha afya Mkowe