Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2017 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 5.0 mwezi Agosti, 2017.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dar es salaam, ambapo amesema kuongezeka kwa Mfumuko huo wa Bei kumechangiwa na kupanda kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.  

 Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na mtama asiliamia 19.8, nazi asilimia 14.8, nyanya asilimia 10.5, mihogo asilimia 11.5, na Mchele asilimia 9.7.

 Aidha, baadhi ya bidha zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa Bei ni pamoja na mkaa asilia 13.9, kodi za nyumba na makazi binafsi asilimia 6.3 na mabegi ya shule asilimia 9.4. 

 Hata hivyo, ameongeza kuwa, uwezo wa Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 92 na senti 18 mwezi Septemba 2017 ikilinganishwa na Shilingi 92 na senti 20 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2017.

 

Video: JPM, Kenyatta wazika vikwazo vya kibiashara, Mawaziri watema cheche
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 10, 2017