Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya Umeme ili kuwa na huduma yenye uhakika.

Ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha huduma ya Nishati hiyo inapatikana kwa uhakika.

Amesema kwasasa serikali imepiga hatua kubwa katika usambazaji wa huduma hiyo, hivyo wananchi hawapaswi kuwa na hofu yeyote.

“Niwahakikishie tu wananchi kwamba serikali ya awamu ya Tano imejipanga vizuri kufikisha huduma hii kwa jamii nzima,”amesema Mgalu

Urusi yadokeza itakachofanya kuhusu mkutano wa Trump na Kim
Mahakama yamshushia ‘mvua’ aliyewaua wazazi wake kwa shoka