Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Neema Mgaya amewataka wabunge wa vyama vya upinzani kuacha kujifunga Plasta midomoni wakati bunge linapokuwa katika vikao vyake.

Mgaya amesema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kufanya hivyo ni kuwakosea wananchi ambao ndiyo wapiga kura wao waliowachagua kwa lengo la kutafuta utatuzi wa kero zao na kuwaletea maendeleo.

Amevishauri vyama vya upinzani kushindana kwa hoja na si kuziba midomo kwa Plasta na kususia vikao, ambapo amebainisha kuwa vitendo hivyo havina tija.

“Unajua kwamba wabunge wote wamechaguliwa na wananchi, hivyo kuziba midomo au kususia vikao ni kutowatendea haki wapiga kura wao,” amesema Mgaya

 

Maua Sama: Ngumu kusahau, zilikuwa siku ngumu katika maisha yangu
VAR kutumika 2019 AFC Asian Cup

Comments

comments