Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amina Ally Saguti amesema kuwa kile kilichotokea wakati wa kurudisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi ulikuwa ni mkakati uliokuwa umepangwa.

Ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kulikuwa na kijana ambaye alikuwa amepangwa kwaajili ya kuharibu mchakato mzima.

“Yule kijana alijaribu kunipokonya fomu yangu na kutaka kukimbia nayo, lakini viongozi wenzangu walimdhibiti akashindwa kuichukua, ndipo nilipogundua kuwa kuna mkakati uliosukwa kwa ajili ya kuharibu,”amesema Saguti

 

 

Kesi ya Uchaguzi Zimbabwe: Wapinzani wataja ulawiti kwa mawakala
Video: DC Daqaro awafunda madereva Arusha