Wakili wa kujitegemea, Alex Mgongolwa amesema kuwa misamaha inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa wafungwa ni ya kisheria.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa Katiba inamruhusu rais kutoa misamaha kwa wafungwa.

Amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuingiwa na hofu kwani raisi ana haki na mamlaka ya kutoa misamaha kwa wafungwa wakiwemo viongozi na watu maarufu.

 

 

Makala: Trump na Kim Jong-un, Mtego wa ndege mjanja na tundu bovu
Wanakijiji wawakingia kifua waganga wa kienyeji

Comments

comments