Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja, kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi.

Mafanikio mengine aliyoyataja ni ununuzi wa meli katika ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria pamoja na kufufua Shirika la Ndege la Tanzania ili kuimarisha usafiri wa anga na kukuza sekta mtambuka zikiwemo za utalii, afya, kilimo na kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (SGR).

Majaliwa amesema hayo leo Septemba 14, 2018 Bungeni jijini Dodoma wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, ambapo limeahirishwa hadi Novema 6, 2018.

 

Carb B, Nick Minaj waamsha bifu upya
Bondia Mwakinyo ampiga chini Mayweather, amuomba kitu Rais

Comments

comments