Mwanachama mkongwe wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali amesema kumewakuwa na taarifa mbali mbali katika vyombo vya haabari vinavyomkariri kuwa amekataa mkataba wa Yanga unaotaka kuleta maendeleo ya timu kitu ambacho sio cha kweli.
Amesema makubaliano waliyokubalina kipindi hicho ni kwamba mwekezaji wa kampuni ya Yanga atamiliki asilimia 51 na wanahisa asilimia 49 na sio kuikodisha Yanga kwa kipindi cha miaka kumi, hivyo kitendo cha mwenyekiti wa klabu ya Yanga kubadilisha maamuzi hakiungi mkono licha ya kutaka kuwekeza miaka kumi hata angeomba miezi nane asingetoa timu.
Mzee Akilimali amesema hayo leo Oktoba 21, 2016 jijni Dar es Slaam nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambapo ameeleza kuwa tatizo kubwa liliopo kwa wananchama wa Yanga ni kupenda kupelekwa pelekewa kwani hakuna mkutano hata mmoja unaotoa fursa kwa wanachama kutoa hoja zao badala yake mikutano hiyo inaendeshwa kuhuni akisimama mwenyekiti akielezea wanachama dhamira yake wao wanakubali tu.
 Aidha, mzee Akilimali amedai kutishiwa maisha na wananchama wa Yanga Posta ambao hawatambui majina yao kwa kutishia kumuuwa.
Amesema anapokea jumbe za vitusho kuwa watu watamuuwa, “Wananitukana hadi na mama yangu wanamchanganyisha, na wamesema watanionyesha, nimeamua kwenda kituo cha polisi magomeni kwa ajili ya kutoa ripoti na sasa nina Rb inayonilinda kwa chochote kitakachotokea,” – Mzee Akilimali.

Video: Mfalme wa Morroco kutua Dar na ndege sita kubwa
VPL: Viwanja Sita Kutikiswa Kesho, Viwili Jumapili