Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni CZI, Cyprian Musiba amesema kuwa amekuwa akitishiwa maisha lakini hataacha kumsaidia Rais Dkt. Magufuli.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa amekuwa akichukiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa kiasi cha kumtishia maisha, hatua ambayo imepelekea kuvitaarifu vyombo vya dola ili viweze kuchukua hatua dhidi ya vitisho hivyo.

Amesema kuwa yeye kama Mtanzania mzalendo anaridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli hivyo hataacha kumuunga mkono katika jitihada za kuiletea maendeleo nchi.

“Kupitia kumuunga kwangu mkono Rais Dkt. Magufuli kwa mema na mazuri anayoyafanya, kuna baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa wamekuwa wakinichukia na kuanza kunitolea vitisho, wanasema watanishughulikia, eti kwasababu ya kujitokeza hadharani kumuunga mkono Rais,”amesema Musiba

 

 

Wapinzani walia na hujuma Kata ya Mbagala Kuu
Lema: Suala la haki, usawa na utawala wa sheria sio la Chadema peke yake