Bodi ya utalii nchini imesaini mkataba na Miss Tanzania Queenelizabeth Makune kwaajili ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, mara tu baada ya kuandaa ziara ya kuwatembeza warembo wa miss Tanzania kwa ajili ya kwenda kujionea vivutio.

Mkurugenzi wa bodi ya utalii Tanzania Devotha Mdachi amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuogeza ufahamu wa utalii  kwa warembo wote ili waweze kusimama kama mabalozi kwa kutangaza utalii wa Tanzania.

Aidha bodi ya utalii ilitoa taji la Miss Domestic Tourism kwa ajili ya kutangaza utalii kwenye mashindano ya Miss Tanzania mwaka jana ambapo QueenElizabeth Makune aliibuka mshindi.

Video: Miss Ruaha kuungana na QeenElizabeth kutangaza Utalii
Siri mtoto wa Waziri Msuya kupata ubosi UN

Comments

comments